Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Shoo atoa ujumbe mzito kwa vijana

31140 Askofupic TanzaniaWeb

Wed, 12 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Frederick Shoo amewataka vijana kuacha kushabikia matendo maovu yakiwemo matumizi ya dawa za kulevya, uzinzi na ushoga ili kujenga Taifa lenye hofu ya Mungu

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Desemba 11, 2018 katika wiki ya Askofu na vijana wa kanisa hilo inayoendelea wilayani Karatu.

Amebainisha kuwa kuna tofauti kati ya haki za binadamu na udhalimu, kuwataka vijana kujichunga.

"Msishabikie matendo maovu kwa sababu wanaoyapigia kelele wana pesa nyingi. Msipoteze utu wenu kwa ajili ya mambo yasiyofaa," amesema Dk Shoo.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz