Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Ruwaichi asisitiza umuhimu wa elimu bora

E9b23308b8481a9293183490a9f0feed Askofu Ruwaichi asisitiza umuhimu wa elimu bora

Sat, 12 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

NCHI za Kusini mwa Jangwa la Sahara zina chaguo moja tu la kuwezesha wananchi wake kupata elimu bora, kama zinataka kuendelea na kuondokana na ujinga, umaskini na maradhi.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi kwenye mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha St. Joseph kilichoko Kibamba jijini Dar es Salaam.

Alisema amefurahi kusikia kuwa chuo hicho kinatekeleza mpango wa kuwaandaa wanafunzi kuibua miradi na hatimaye kuisajiri kama kampuni na kutoa ajira kwa vijana wenzao pamoja na kuzalisha bidhaa mbalimbali kibiashara badala ya kuhangaika kutafuta ajira.

“Mpango huu ni muhimu sana na unaendana na mahitaji ya wakati huu ambapo serikali ya Rais John Magufuli inahimiza vijana kujiajiri. Wito wangu kwa menejimenti ya chuo ni kwamba uwekezaji katika mpango huu uongezwe ili wanafunzi wengi zaidi kutoka fani mbalimbali waweze kunufaika nao,” alisema.

Vilevile, alitoa wito kwa vyuo vingine vya elimu ya juu nchini viweze kuja kujifunza kuhusu mpango huo mzuri, ambao alisema utaaongeza idadi ya wahitimu wenye uwezo wa kuanzisha makampuni na hivyo kutengeneza ajira kwa vijana wengi zaidi.

Aliwaasa wahitimu kwamba elimu waliyoipata chuoni waitumie kwa kuitumikia jamii kwa weledi mkubwa, kwa utendaji bora na ufanisi katika fani zao na kwa upande wa madaktari, alisema wanategemewa sana wakatoe huduma bora kwa wananchi katika kupigana na adui maradhi.

“Ninawaasa wahandisi mkawe wabunifu na kuutumia ujuzi mlioupata kufanikisha lengo la serikali la kuifanya Tanzania iwe na uchumi unaotokana na maendeleo katika viwanda kwa kufanya kazi katika sekta rasmi au katika sekta isiyo rasmi,” alisema

Alitoa wito kwa watanzania kutumia chuo hicho cha St Joseph kwa kuwa ni Chuo pekee kinachotoa elimu ya juu na kusisitiza nidhamu ya hali ya juu kwa wanafunzi wake pamoja na Jumuiya yake yote.

Aliwahimiza wanafunzi wanaoendelea na masomo chuoni, kutumia muda wao vizuri na wasome kwa bidii ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea kwa mafanio yao wenyewe, jamii na taifa kwa ujumla.

Chanzo: habarileo.co.tz