Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Ruwai’chi kuongoza misa ya kitaifa ya Pasaka

4ab258f96318e0739b92286e11a5b32b Askofu Ruwai’chi kuongoza misa ya kitaifa ya Pasaka

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MISA Takatifu ya adhimisho la Pasaka Kitaifa inafanyika leo katika Kanisa la Bikira Maria wa Fatima, Parokia ya Msimbazi, Jimbo Kuu la Dar es Salaam na itaongozwa na Askofu Mkuu wa jimbo hilo, Yuda Thadeus Ruwai’chi.

Taarifa ya Baraza la Maaskofu (TEC) iliyotolewa jana na Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Padre Chesco Msaga, ilisema kuwa Misa hiyo itaanza saa 2:45 asubuhi.

Padre Chesco alisema Ibada hiyo ya Misa Takatifu itarushwa mubashara na vyombo vya habari vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ikiwamo televisheni ya TBC1 na radio TBC Taifa pamoja na vyombo vya kanisa ambavyo ni Radio Maria na Radio Tumaini.

Ibada ya kitaifa ya Ijumaa Kuu iliadhimishwa kitaifa juzi katika Kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiongozwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa.

Dk Malasusa alitoa mwito kwa Wakristo kote nchini kujitoa kwa moyo leo kumuomba Mungui nchi iendelee kuwa na amani, upendo na mshikamano huku akiwakumbusha pia kumuomba Mungu awape viongozi wapya hekima ya kuongoza kwa haki.

Awali akisoma neno la tatu na nne kati ya maneno saba ya Yesu msalabani, Mchungaji Anyingisye Mshami wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema pamoja na kuwa nchi iko kwenye majonzi ya kufiwa na hayati Rais Magufuli na wapendwa wengine,Yesu Kristo anataka watu wasikate tamaa kwa sababu yeye ameshinda kifo.

Aidha katika mahubiri yake aliwataka Wakristo kutoogopa kufa bali wajiandae muda wote kwa kuhakikisha wanafanya matendo mema kwani Kristo alishinda na msalaba kwa wakristo ni alama ya ushindi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz