Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Pengo azungumzia mapokezi ya Ruwa’ichi

14366 Pic+pengo TanzaniaWeb

Tue, 28 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam wa Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewaalika waumini wa dhehebu hilo kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Askofu Mkuu mwandamizi, Yuda Thadeus Ruwa'ichi.

Taarifa ya Katibu wa jimbo hilo, Padri Frank Mtavangu iliyotolewa jana Jumatatu Agosti 27, 2018 inaeleza kuwa mapokezi hayo yatafanyika Ijumaa Septemba 7, 2018.

Juni 2018, Papa Francis wa 16 alimtangaza Ruwa’ichi kuwa askofu mkuu mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Padri Mtavangu amesema katika kufanikisha mapokezi hayo, “Kardinali Pengo anatualika wote kushiriki katika mapokezi haya. Askofu mkuu mwandamizi atapokelewa rasmi kijimbo kwa adhimisho la misa takatifu itakayoanza saa 10:00 jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu.”

 

“Mara baada ya misa kutakuwa na hafla fupi ya chakula cha jioni katika viwanja vya shule ya sekondari na msingi ya Millenium (zamani Forodhani) ambapo maklero wote na wawakilishi wa rnakundi mbalimbali watashinki.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz