Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Mwanisongole Kuzikwa Leo Songwe

MWANISONGOLE (6) Askofu Mwanisongole Kuzikwa Leo Songwe

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askofu Mkuu Mstaafu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Ranwell Mwanisongole aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi, Desemba 25, 2021 katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam anatarajiwa kuzikwa leo Vwawa mkoani Songwe.

Taarifa kutoka kwa familia hiyo, zinaeleza kuwa Dk. Mwenisongole ambaye pia ni baba mzazi wa Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole, atazikwa katika makaburi ya familia yaliyopo Ichenjezya, Vwawa wilayani Mbozi na kwamba maandalizi yote tayari yamekamilika.

Desemba 26, 2021 Rais Samia Suluhu Hassan alitoa salamu za pole kwa familia ya Mwenisongole na kueleza kwamba ameshtushwa na taarifa za kifo cha mchungaji huyo aliyekuwa akiliongoza Kanisa la TAG Upanga jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live