Serengeti. Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael Msonganzila amesema matumizi ya kondumu hayawezi kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), kuwataka wananchi kumrudia Mungu.
Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 6, 2019 wakati akitoa sakramenti ya kipaimara kwa waamini 192 wa parokia ya Mugumu Serengeti.
Amesema tathmini itatakiwa kufanyika kubaini sababu za ongezeko la maambukizi hayo kwa maelezo kuwa kampeni za mabilioni ya fedha zinafanyika lakini maambukizi bado yapo.
"Watu wamepumbazwa na matumizi ya kondomu kama kinga kumbe inawachochea kufanya zinaa zaidi na matokeo yake maambukizi yanazidi na waathirika wakubwa ni wanawake" amesema.
Askofu amesema matumizi ya kondomu hayakubaliwi na kanisa hilo, kwamba halipingani na Serikali na Serikali kuhusu matumizi yake, “Bali (kanisa) linaangalia kwa undani athari za kuwaaminisha watu kuwa ni kinga.”
Amesema wasichana wenye umri mdogo baadhi wamekuwa na matatizo kwa kuingia katika ndoa wakiwa wadogo jambo alilodai kuchangia maambukizi.
Pia Soma
- Magufuli amtaka IGP Sirro kumsimamisha kazi kigogo polisi
- Magufuli azindua barabara akishangaa wingi wa matuta
- Magufuli atoa siku tano Tanroads kuhamisha ofisi zao, zingine mwezi mmoja
Amewataka wazazi kuachana na tabia ya kulazimisha kuwaoza watoto wao kwa ajili ya tamaa za kujipatia mali.
“Ndoa ni tendo la hiari kikanisa na kiserikali, acheni tabia hizo watoto waweze kusoma na kufikia malengo yao,” amesema.