Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Mkuu: Wasikilizeni wagombea mfanye uamuzi

5b9d10595d4134c0e1578e0974a75a55 Askofu Mkuu: Wasikilizeni wagombea mfanye uamuzi

Mon, 14 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATANZANIA wameshauriwa kuwasikiliza wagombea wa vyama vyote kwa usawa ili wachague mtu atakayeimarisha amani, haki, umoja na mshikamano na kuwaletea maendeleo.

Wito huo ulitolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda-Thadei Ruwa’ichi, katika Misa Takatifu ya Kutukuka kwa Msalaba, iliyofanyika katika kanisa la Hija, Parokia ya Pugu, jimboni humo.

“Ni vizuri watu wawasilikilize wagombea wote wanapotoa sera ili Oktoba 28 wafanye uamuzi sahihi.” “Si vema kumpuuza mgombea hata mmoja, kwani katika kuwasilikiza mpiga kura anaweza kufanya uamuzi sahihi wa kuchagua mtu atakayesimamia amani ya nchi, haki, umoja, mshikamano uliopo na atakayewaletea maendeleo,” alisema.

Askofu Mkuu Ruwa’ichi alihimiza wagombea na vyama vyao kuendesha kampeni za kistaarabu, amani na utulivu na kunadi sera badala ya kutoa maneno mabaya kwani Watanzania watawapima kwa namna wanavyozungumza.

“Tuendelee kumuomba Mungu aibariki na kuilinda nchi yetu iendelee kudumu katika amani, haki, kuheshimana na kuthaminiana na katika kuzingatia yanayompendeza,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.

Wagombea wa vyama vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu wanazunguka katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kampeni za urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Chanzo: habarileo.co.tz