Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Mkuu Kinyaiya awapa neno wenye uchumba sugu

Fca724b05b1859384288f18870c23c5e Askofu Mkuu Kinyaiya awapa neno wenye uchumba sugu

Tue, 22 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Beatus Kinyaiya (pichani) amewataka waumini wanaoishi uchumba sugu, kufunga ndoa ili kuzipokea neema na baraka za Mungu katika maisha yao.

Akihubiri katika Parokia Mpya ya Mtakatifu Isidori Mkulima Dodoma Makulu, Askofu Kinyaiya alisema moja ya mafanikio ya kanisa lolote ni waumini wake kuzipokea neema za Mungu na kuzitumia katika maisha yao.

Aliwataka wanakwaya, ambao wengi wao wanaimba vizuri lakini hajawajafunga ndoa, kufunga ndoa ili kuleta neema katika maisha yao. Kinyaiya aliwataka wanandoa wapya waliofunga siku hiyo kuwa wajumbe.

Aliwashauri waumini wengine ambao wanaishi uchumba, wafunge ndoa na kuzipokea neema za Mungu katika maisha yao.

Askofu huyo aliwataka viongozi wa parokia mpya kutoka katika jumuiya na viongozi wa parokia kuwa wajumbe, kwenda kuwashauri wote wanaoishi uchumba sugu kufunga ndoa zao ili kuifanya parokia mpya ing’are.

Akitangaza parokia mpya ya Mtakatifu Isidori Mkulima Dodoma Makulu na paroko wake, Padri Jonas Mlewa, Askofu Mkuu Kinyaiya alisema ni parokia changa lakini inatakiwa kukimbia na kuzipita parokia zawaswa, Ilazo na Parokia mama ya Makole.

Akimsimika paroko mpya, Padri Mlewa, Askofu alimtaka padri huyo kuitetea imani yake, kuitangaza injili na kutoa sakramenti zote kwa waumini wa parokia hiyo.

Akizungumza Padri Kiongozi wa Dekania ya Mtakatifu Petro, Padri Antipashayo aliongoza Parokia za Dekania hiyo ikiwemo Parokia mama ya Makole, Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Ilazo, Ihumwa,waswa na Parokia teule ya Nzuguni, kuisaidia parokia hiyo mpya hiyo kwa kuipa vifaa vya nyumba ya padre iweze kusimama na kujitegemea.

Paroko mpya Mlewa aliwapongeza waumini wa parokia hiyo kwa mshikamano, waliouonesha katika kujenga nyumba ya padri, kujenga ukumbi na kufanikisha sherehe ya uzinduzi wa parokia yao.

Katibu wa Parokia hiyo, Josephanka alikisoma taarifa ya parokia hiyo, alisema ilianza kuwa Kigango mwaka 2010, ikawa Parokia Teule tangu Januari 19, 2020 na sasaeptemba 20, 2020 ni Parokia kamili.

Pamoja na uzinduzi wa Parokia Mpya ya Dodoma Makulu, pia Askofu Mkuu Kinyaiya alifungisha ndoa tatu, alitoa kipaimara kwa vijana 18 na komunyo ya kwanza kwa vijana 38.

Chanzo: habarileo.co.tz