Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Kilaini awapongeza kina Majaliwa ajali ya ndege

KILAINIII WEB Askofu Kilaini awapongeza kina Majaliwa ajali ya ndege

Mon, 14 Nov 2022 Chanzo: eatv.tv

Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Bukoba, Method Kilaini amepongeza ushirikiano uliooneshwa baina ya wavuvi (kina Majaliwa) na serikali wakati wa zoezi la uokoaji wa wahanga wa ajali ya ndege ya Precision Air, iliyotokea Novemba 06, 2022 mkoani Kagera.

Askofu Kilaini amesema hayo mkoani Mwanza wakati akizungumzia ajali ya ndege ya Precision Air ambapo amesema ajali ni tukio lisilozuilika pindi inapotokea bali ni mpango wa Mungu, hivyo hatua ya kuokolewa abiria 24 kwenye ajali ya ndege ni jambo la kupongezwa kwa kuwa bila ya kuwepo ya jitihada za kutosha za Serikali na Waokoaji abiria wote 43 wangefariki.

"Ajali huwa haina kinga pindi inapotokea, ila jambo la kwanza ninalopenda kushukuru ni Watanzania kuonesha mshikamano na umoja na mpaka imepelekea kuokolewa kwa watu 24 kwangu mimi nauita ni muujiza tunapaswa sana kumshukuru Mungu," amesema Askofu Kilaini.

Chanzo: eatv.tv