Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Katoliki ataka waumini kusamehe, kutolipa visasi

Askofu Katoliki ataka waumini kusamehe, kutolipa visasi

Sun, 24 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Waamini wa Kanisa wa Katoliki nchini Tanzania wanatakiwa kusamehe, kuwachukulia wenzao vema, kuwapatanisha na kutolipa kisasi ndiyo njia ya kuwafikisha mbinguni.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Novemba 24, 2019 na Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma mkoani Mara, Michael Msonganzila katika mahubiri ya Misa iliyofanyika Kanisa la Kristo Mfalme Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Asizi.

Amesema Yesu Kristo pamoja na kuwa na nguvu ya kimungu aliwasamehe waliomtesa, kumkebehi na hata kumuua kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kumfikia Mungu.

"Sisi ni nani hatuwezi kusameheana, kusikilizana, kuvumiliana na kuwaheshimu wengine halafu tukijidai kuwa tutauona Ufalme wa Mungu, lazima kila mmoja afanye mageuzi ndani ya moyo wake," amesema Askofu Msonganzila

Amesema Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuwa heri wapatanishi hao wataitwa wana wa Mungu, heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki maana ufalme wa mbinguni ni wao kuwa mafundisho hayo yana maana kubwa kwa kila mmoja.

"Ufaransa kulikuwa na mfalme ambaye alisema serikali ni yeye na Italia alikuwepo aliyesema Mungu ameweka amri kumi yeye akaweka zake 13 ya kwanza akidai kuwa mfalme hakosei, haya ni mambo ya kutaka kujitukuza kidunia na kumsahau Mungu," amesema.

Kiongozi huyo wa kiroho amesema moja ya kuvunja amani, umoja na mshikamano wa nchi ni watu kutaka kuwa juu ya Mungu, kutokuwasamehe wenzao wanapokuwa wamekosana  kama waamini na nchi fundisho kubwa ni jinsi Yesu alivyowachukulia watesi wake kwa upole.

"Sisi tuna kitu gani cha kujiona bora kama wanafunzi wa Yesu kama Petro aliyemkana mara tatu lakini alipotambua makosa alitubu na mwisho alimwachia imani kubwa, kwa waliona nafasi wanatakiwa kuwavumilia walioko chini na kuwasikiliza, hapo tunaishi katika heri walizofundishwa wanafunzi wake," amesema.

Amesema nafasi walizonazo watu zinapita kama ilivyotokea kwa mfalme wa Ufaransa, Italia, Bukinafaso na wengineo lakini katika ufalme wa Mungu wanakuwa wamejiweka pabaya.

Chanzo: mwananchi.co.tz