Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Kakobe asikitishwa wanaomtukana mitandaoni

38784 Kakobe+pic Askofu Kakobe asikitishwa wanaomtukana mitandaoni

Tue, 29 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe ameeleza kusikitishwa na maoni ya watu wanaomtukana kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuhudhuria mkutano uliotishwa na Rais John Magufuli hivi karibuni.

Alisema tangu alipoanza kuhudhuria hafla ambazo Rais Magufuli anaalikwa, watu wengi wamekuwa na maoni tofauti, baadhi wakimhusisha na Chadema au ameahidiwa ubunge au nafasi serikalini na wengine wakidai amenunuliwa.

Askofu Kakobe akijibu hoja hizo jana huku akitetea uamuzi wake wa kuhudhuria hafla hizo na kumuombea Rais Magufuli, alisema viongozi wa dini wanastahili heshima kwa sababu ni walezi wa kiroho watu.

Kuhusu kuhusishwa na Chadema, Askofu Kakobe alikana na kusisitiza kuwa kanisa lake halina chama na hakuwahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Hata hivyo, mkurugenzi wa itikadi wa Chadema, John Mrema alisema hakuna kiongozi wala mwanachama aliyetukana viongozi wa dini bali anajua wananchi wamewakosoa viongozi hao.



Chanzo: mwananchi.co.tz