Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Kakobe amfagilia Magufuli kwa kutobagua madhehebu ya dini

37260 Askofupic Askofu Kakobe amfagilia Magufuli kwa kutobagua madhehebu ya dini

Fri, 18 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema kufanikiwa kwa mataifa makubwa kunatokana na kumtanguliza Mungu mbele katika kila shughuli wanayoifanya.

Ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) iliyofanyika katika Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania(TCRA) jijini Dar es Salaam.

Askofu Kakobe amesema jambo hilo limeweza kudhihirika hata kwa nchi ya Marekani kwani uthubutu wao wa kuweka maneno ya Mungu In God We Trust (Tunamuamini Mungu) katika dola yao kumeifanya pesa hiyo kuwa na thamani na kutumika dunia nzima.

“Umeanza vyema Rais John Magufuli kwa kumtanguliza Mungu katika shughuli unazozifanya, Mungu ameandaa baraka na zitakapokuja hakuna anayeweza kuzizuia,” amesema Askofu Kakobe.

“Haijawahi kutokea kuwa na Rais na Serikali yake ambao wameheshimu viongozi wa dini kama wewe, si kwa viwango hivi kwa sababu katika uongozi wako hakuna dhehebu kubwa wala dogo wote wameheshimiwa sawa, suala hilo ni ufunguo kwa baraka zinazokuja,” ameongeza.

Naye Askofu mkuu wa kanisa la Wapo International, Sylvester Gamanywa amesema ucha Mungu na utii ulio ndani ya Rais Magufuli ndio umefanya kuweka kipaumbele kwa dini na sala katika shughuli zote anazofanya.

“Mungu amekuinua na atakuinua kwa unyenyekevu wako,” amesema Gamanywa.



Chanzo: mwananchi.co.tz