Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Kakobe: Dhambi imeleta mafarakano katika familia

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema dhambi imeleta mafarakano katika familia jambo ambalo limesababisha watu kutengana na kusababisha watoto kuteseka.

Akihubiri kwenye ibada ya Krismasi leo Jumanne Desemba 25, 2018 iliyokuwa na ujumbe usemayo 'Yesu ni mwokozi wa Ulimwengu,’ Kakobe amesema dhambi inawatesa watoto baada ya wazazi kufarakana jambo ambalo limesababisha mpasuko mkubwa katika familia.

Askofu Kakobe amewataka watu wamuombe Mungu ili aweze kuwaondoa katika dhambi ambayo imetawala duniani na imekuwa chukizo.

Amesema utakuta vitendo vya ushoga, ulawiti na ubakaji vimeongezeka hali hiyo inatisha kama enzi ya Sodoma na Gomora hivyo watu wanatakiwa kumtumikia Mungu kwa imani na kiroho.

"Mungu wetu hataki kutuona tunasherehekea Sikukuu ya Krismasi bila ya kujua maana bali mnatakiwa kufahamu maana yake ili muweze kukombolewa katika dhambi ," amesema.

"Dini haiwezi kumsaidia mtu kupambana na dhambi wengine wanatumia miavuli kuyaficha mambo yao hivyo unatakiwa kumkimbilia Mungu ili aweze kukuokoa," amesema Askofu Kakobe.

Askofu Kakobe amesema leo hii yapo matukio duniani yanafanyika lakini watu hawaogopi utakuta watu wanafungwa magerezani huku wengine wanapigwa risasi lakini dhambi zimeendelea kuongezeka.



Chanzo: mwananchi.co.tz