Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu: JPM amejenga historia

7d6ee2b3017fb731aa4ed64fa1bdb148 Askofu: JPM amejenga historia

Thu, 12 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ASKOFU Mkuu wa Huduma ya The World Ministries,DamasThadey amempongeza Rais John Magufuli kwa kuandika historia kubwa kutokana na uamuzi wake wa kuamua sherehe za kuapishwa kufanyika kwa mara ya kwanza makao makuu ya serikali Dodoma.

Pongezi hizo zimetolewa na kiongozi huyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa baada ya kumalizika kwa ibada iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo lililopo Dodoma Makulu.

Askofu huyo alisema uamuzi wa Rais Magufuli wa kuamua sherehe za kupishwa kufanyika makao makuu ya nchi ametengeneza ukurasa mpya wa utawala wake ambapo huko nyuma shughuli hizi zilikuwa zikifanyika mkoani Dar es Salaam.

Hata hivyo amemuomba rais atakayechukua kijiti cha Magufuli baada ya kumaliza muhula wake, kuhiheshimu hatua hiyo ya kufanyia sherehe ya kuapishwa Dodoma, hii ikiwemo na zingine zote za kitaifa ili kuleta maana halisi ya uwepo wa makao makuu ya nchi.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la International Evangelism Sinai Ipagala mkoa wa Dodoma, Selvester Thadey, amewataka watanzania kuliombea Bunge ili waweze kutekeleza maamuzi yao bila kuangalia itikadi ya chama.

Alisema kuwa ni matarajio makubwa ya watanzania kuona maendeleo zaidi yanapatikana kwenye majimbo wanayotoka hata kama mengine yalikuwa yakiongozwa na vyama vya upinzani na ili waweze kufanikiwa wanahitajika kuombewa.

Chanzo: habarileo.co.tz