Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Gwajima ampa ushauri Rais Magufuli kuhusu madini

37875 Pic+gwajima Askofu Gwajima ampa ushauri Rais Magufuli kuhusu madini

Tue, 22 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Joseph Gwajima amemshauri Rais John Magufuli kuwashirikisha wataalamu wa madini badala ya wasomi pekee.

Askofu Gwajima ametoa ushauri huo leo kwenye mkutano mkuu wa kisekta uliomkutanisha Rais John Magufuli na wadau wa madini.

Kiongozi huyo wa kidini amesema siyo kweli kuwa hakuna soko la madini kwa sababu dhahabu yenyewe ni fedha isipokuwa kushirikisha wasomi pekee wasiokuwa na asili ya madini kunachangia kupoteza fedha nyingi.

Amesema kuwe na wataalamu wa madini wenye kujua siasa za biashara ya madini hususan wale waliotoka kwenye mikoa yenye rasilimali hiyo bila kujali ni msomi au la.

"Rais unaweza kuunda watu wenye akili na ‘exposure’ ya madini ambao wanaweza kuzifika nchi mbalimbali duniani kuyafikia masoko ya vito kama rubi, wasiwe wasomi wawe wataalamu wa madini," amesema.

Amesema hataki ushuru upungue bali mfumo wa utozaji ushuru ubadilike kwa sababu wachimbaji wadogo wanaonewa.

Amesema kukiwa na kituo cha mauzo,  mchimbaji mdogo asilipe bali auze, ila mwenye kituo cha mauzo ndiyo alipe.

Ameeleza aliwahi kupita Maganzo Shinyanga akaulizwa aletewe almasi akakubali ndani ya saa moja aliletewa bakuli zima na akaambiwa wanazo ndani.

"Kama kutakuwa na utaratibu wa kubadili mfumo wa hizi tozo kwa wachimbaji wadogo Serikali itapata fedha nyingi" amesema Gwajima.

Kabla ya kuzungumza Gwajima amesema kuwa angeshangaa sana kuondoka kwenye mkutano huo bila kuzungumza.



Chanzo: mwananchi.co.tz