Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Gamanywa ashauri elimu ya uraia kanisani

D52a7933a7cdde5c85d7fe369bbe8dd0 Askofu Gamanywa ashauri elimu ya uraia kanisani

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ASKOFU Mkuu wa WAPO Mission International, Silvester Gamanywa amewataka maaskofu na wachungaji kufundisha elimu ya uraia katika makanisa yao badala ya siasa hasa wakati huu wa mchakato wa mandalizi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Alisema hayo jana wakati akihubiri kanisani katika Kanisa la BCIC- Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, na kusisitiza kuwa, baadhi ya Wakristo na jamii kwa jumla nchini wanadhani kuwa viongozi wa dini kufundisha uraia na uzalendo makanisa ni kosa na kwamba hiyo ni dhana potofu.

Alisema, viongozi wa kiroho ni sehemu ya jamii na kwamba moja ya majukumu yao ni kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo katika kipindi chote cha kujiandaa kwa uchaguzi mkuu.

“Kama kuna watu wanaumia kuona tunaongea hicho wanachokiita siasa kanisani ni kukosa elimu ya uraia; ni sawa na kukosa maarifa kwa kuwa hata Yesu Kristo mwenyewe alikuwa akifundisha elimu ya uraia na uzalendo ndiyo maana alielekeza wanafunzi wake kulipa kodi na kumpa Kaisari yaliyo yake Kaisari na kumpa Mungu yake Mungu,” alisema Gamanywa.

Alisema, kipindi hiki cha kampeni mpaka uchaguzi mkuu kumalizika, kila mmoja anapaswa kuonesha uzalendo wake kwa vitendo huku jamii ikiendelea kukumbushana masuala muhimu ya elimu ya uraia.

Askofu Gamanywa alisema, huu si wakati wa kufanya mijadala zikiwemo siasa kanisani, bali kuombea nchi huku kila kiongozi wa dini akihakikishe anafundisha waumini wake elimu ya sahihi kuhusu uraia.

Kiongozi huyo wa kiroho anajiandaa kuzindua kitabu alichokiandika hivi karibuni kinachoitwa Uzalendo na Falsafa ya Mamlaka ambacho kitakachofundisha uzalendo na elimu ya uraia.

Chanzo: habarileo.co.tz