Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Chilogani ataka Watanzania kuchagua viongozi wacha Mungu kama Magufuli

102232 Pic+magufuli Askofu Chilogani ataka Watanzania kuchagua viongozi wacha Mungu kama Magufuli

Mon, 13 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT), Dk Dickson Chilongani amesema katika uchaguzi wa mwaka 2020, ni vema Watanzania wakawachagua viongozi wacha Mungu huku akimtaja Rais John Magufuli kuwa ni mcha Mungu.

Askofu Dk Chilongani ametoa kauli hiyo leo Jumapili Aprili 12, 2020 wakati akihubiri katika ibada ya pasaka iliyofanyika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu jijini Dodoma. Dk Chilongani alianza kwa kumshukuru Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kutokuzuia ibada makanisani akisema amefanya hivyo kwa sababu ni mcha Mungu hivyo akawaomba Watanzania kumuombea na kumuunga mkono.

Askofu amesema kuwaruhusu waumini waendelee kukutana na kusali kwa pamoja ni jambo jema linalopaswa kupongezwa na watu wote kwani wanapata nafasi ya kumlilia Mungu kuhusu janga kubwa la corona ambalo limeikumba dunia.

“Rais Magufuli ni kiongozi wa mfano anayepaswa kuigwa na dunia, kitendo cha kutupa nafasi sisi tuendelee kumlilia Mungu katika makanisa ni cha kuungwa mkono, hivi mbona huko waliozuiwa kusali nako bado maambukizi ni makubwa tu, lakini nasisitiza tuendelee kufuata ushauri wa wataalamu wetu wa afya,” amesema Dk Chilongani.

Amesema bado ulimwengu wote unaishi katika nguvu za giza na ndiyo maana Mungu anaendelea kufanya matengenezo kila wakati hivyo magonjwa kama corona na mengine hayana budi kutokea.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu amesema ni wakati kwa Watanzania kuangalia viongozi wacha Mungu wasioegemea kwa waganga wa jadi kwani wanaweza kulipeleka kubaya Taifa.

Huku akisisitiza kuwa hampigii debe Rais Magufuli lakini aliyarudia maneno yake kuwa ni kiongozi mcha Mungu wa kweli anayejua anachokifanya.

Chanzo: mwananchi.co.tz