Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Cheyo amtaka Magufuli kutoa ajira kwa vijana

38031 Pic+morovian Askofu Cheyo amtaka Magufuli kutoa ajira kwa vijana

Wed, 23 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi, Alinikisa Cheyo  amemtaka Rais wa Tanzania, John Magufuli kutoa nafasi za ajira kwa vijana kwani kutofanya hivyo kunaweza kuwasababisha kuingia katika mambo maovu.

Askofu Cheyo ameyasema hayo leo Jumatano Januari 23, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam katika mkutano kati ya Rais Magufuli na viongozi wa madhehebu ya dini.

Amesema wapo baadhi ya wahitimu ambao fani walizosomea zinawaruhusu kujiajiri bila matatizo yoyote lakini wapo pia wahitimu ambao fani zao haziwaruhusu kufanya hivyo.

“Tayari umeshaondoa watumishi hewa, walio na vyeti feki ni jambo ambalo linapaswa kusifiwa na kujivunia kama nchi hivyo umefika wakati sasa wa wewe kuwaangalia vijana wetu waliohitimu,” amesema Cheyo na kuongeza:

“Wapo vijana wengi ukienda vijijini utakuta wamemaliza vyuo lakini hawana kazi yoyote ya kufanya, angalau hata sisi tuliosoma wakati wa awamu ya kwanza tulifundishwa namna ya kujitegemea bila kuajiriwa.”

Naye Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Amani Lymo amesema licha ya kuanzishwa kwa elimu bure lakini kuna changamoto zinaikabili sekta hiyo na ameomba kuruhusu michango pale inapohitajika.

“Bodi ya shule ziruhusiwe basi kukaa ili kujua kitu gani wanaweza kukitekeleza kwa kutumia nguvu ya wananchi ili kuhakikisha elimu inakuwa siyo bure tu bali iliyokuwa na ubora,” amesema.

Pia, amesema waziri wa afya afanye uchunguzi kuangalia namna ya kuwasaidia watu wanaoishi katika hali ya chini kwani licha ya kuwapatia bima kuna sehemu hazikubaliki.

“Ulishuhudia kile kilichotokea KCMC tunaomba changamoto kama hizi zitafutiwe ufumbuzi ili kuhakikisha kuwa kile mtu alichokilipia anakitumia vyema na kunufaika nacho,” amsema.



Chanzo: mwananchi.co.tz