Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Bagonza ataja makundi 14 yasiyo na furaha

85777 Pic+bogonza Askofu Bagonza ataja makundi 14 yasiyo na furaha

Mon, 25 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Askofu wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Benson Bagonza ametaja makundi 14 ya watu anaodai hawana furaha kutokana na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini Tanzania uliofanyika jana Jumapili Novemba 24, 2019.

Askofu Bagonza ametoa andiko jipya leo Jumatatu Novemba 25, 2019, ikiwa ni siku moja baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao kwa sehemu kubwa wagombea wa chama tawala CCCM wamepita bila kupingwa maeneo mengi.

Katika andiko lake hilo ambalo linasambaa katika mitandao ya kijamii ikiwamo makundi ya WhatsApp, Askofu Bagonza  anasema waliopiga kura hawana furaha na waliosusa au kususwa hawana furaha.

Anasema waliopita bila kupingwa nao hawana furaha, waliosimamia kura hawana furaha, walioshinda hawana furaha na hata walioshindwa hawana pia furaha na uchaguzi huo.

Katika andiko hilo, Askofu Bagonza anasema waliopanga yaliyotokea hawana furaha, waliopangiwa yaliyotokea hawana furaha na walioshauri hekima hawana furaha.

Anasema kutokana na uchaguzi huo, waliokaa kimya hawana furaha, wanaounga mkono nilichoandika hapa hawana furaha na wanaopinga anachoandika hapa, hawana furaha.

“Wanaodhani wana furaha pia hawana furaha. wapinzani hawana furaha, wapinzani wa wapinzani, hawana furaha. Wanaodhani hawana furaha ni kweli hawana furaha na kuhoji furaha yuko wapi,” anasema

Uchaguzi wa serikali za mitaa umefanyika jana Jumapili huku vyama sita vya upinzani vikisusia uchagizi huo ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, UPDP, Chaumma na ACT- Wazalendo.

SOMA ZAIDI

Chanzo: mwananchi.co.tz