Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Bagonza aingia katika Ubunge wa Lissu na maswali tata

64844 Askofu+pic

Sat, 29 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza amezungumzia suala la Tundu Lissu kupoteza sifa za kuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) kwa kuhoji tofauti ya Bunge na bonge.

Jana Ijumaa Juni 28,2019 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alilieleza Bunge la nchi hiyo kwamba Lissu amepoteza sifa za kuwa mbunge kwa sababu ya kutokujaza fomu za mali na madeni ya maadili ya viongozi wa umma na kutokutoa taarifa kwake (Spika) aliko.

Spika Ndugai alisema hafahamu Lissu yuko wapi na amekuwa akimwona katika vyombo mbalimbali vya Kitaifa na Kimataifa akizungumza masuala mbalimbali huku bungeni akiwa haonekani hivyo kumwandikia barua mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi kumweleza kiti cha Lissu bungeni kiko wazi.

Kupitia akaunti yake ya Facebook ambao Mwananchi lilipotaka kupata maoni yake kuhusu suala hilo la Lissu, Askofu Bagonza amesema ujumbe uliopo Facebook ndio maoni yake.

Ujumbe huo wenye kichwa cha habati ‘Kuna tofauti kati ya Bunge na Bonge.’

“Bunge huongozwa kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni, tamaduni za mabunge, mila na desturi nzuri, busara na hekima.

Pia Soma

Askofu Bagonza anasema, “kikikosekana kimoja hapo juu, linageuka kuwa bonge. Maana yake, bonge linatisha, linaonea, linapendelea, linajichanganya, linahujumu, linajihujumu, linalipiza kisasi, linakera na halina utu wala huruma.”

“Bunge letu siyo bonge. Mungu Ibariki Tanzania. Libariki Bunge letu. Liepushe na majaribu ya kuwa bonge.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz