Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anusurika kuteketea kwa moto wakati akiombewa na mchungaji ili kuondoa pepo

54624 Pic+kuungua

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Philipo Elias (22)mkazi wa Kakonko Kigoma amelazwa hospitali Teule ya Nyerere wilayani hapa akiwa na hali mbaya baada ya kuchomwa moto na mchungaji wake kwa madai ya kufukuza nguvu za giza.

Tukio hilo linalotajwa la kwanza kupokelewa hospitalini hapo likihusisha imani za kidini linadaiwa kutokea Aprili 28,mchana katika kanisa la Cag Calvari katika kijjji cha Musati limethibitishwa na uongozi wa kijiji na hospitali hiyo.

Akiongea na Mwananchi digital leo Jumatatu Aprili 29 majeruhi hospitalini alikolazwa amesema alienda kuombewa kwa kuwa anasumbuliwa na kichwa.

Anasema aliambiwa kupiga magoti na afumbe macho  na kutii ndipo akamwagiwa mafuta ya taa na wakawasha moto na kuanza kuungua huku wakiomba kuwa mizimu yote itakwisha na atapona.

"Nilianza kuungua huku wao wakizidi kuomba, hali  ikawa ngumu nikapiga kelele ndipo wakaanza kuuzima moto huku wakisema hiyo ni nguvu ya Mungu, watu wakaanza kujitokeza nikapelekwa Kituo cha Polisi Kenyana na kukimbizwa hapo hospitali kwa matibabu.

Elias ambaye anafanya kazi za kuchunga mifugo kwa Thomas kazi ambayo ameianza mwezi Februari anasema kilichofanywa si maombi bali walitaka kumuua kwa kuwa kumwagia mafuta ya taa na kuwasha moto hakujawahi kufanyika hapo kanisani.

Mchungaji Anna Butoke akiongea kwa simu na Mwananchi digital aprili 29 amekiri kuwa wao walikuwa wanachoma mikoba ya kijana huyo ajabu akawa anaungua yeye.

" Alifika kujaribu kutaka kuteketeza mchungaji na viongozi wengine lakini akazidiwa nguvu, tukamwambia alete vifaa vyake vya uchawi, tukavimwagia mafuta ya taa na kuwasha moto akiwa amevishika badala ya kuungua vifaa hivyo akawa anaungua yeye nasi tulishangaa, "amesema.

Muuguzi wa zamu John Nyang'ombe amesema hali yake si nzuri sana kwa kuwa athari za moto ni nyingi na wanajitahidi kumwekea maji mara kwa mara na dawa za kuzuia maambukizi mengine ya ngozi.

Kamanda wa polisi wilaya ya Serengeti Methew Mgema amesema wanafuatilia undani wa tukio hilo na kuwa watuhumiwa wote watakamatwa ili waweze kuhojiwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz