Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayedaiwa kumuua mwanakwaya gesti akamatwa

16313 Akamatwa+pic TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtu anayedaiwa kumuua Mariam Charles (22), mwanakwaya wa Kanisa la AICT, Chang’ombe amekamatwa leo Jumamosi Septemba 8, 2018.

Mtu huyo amekamatwa wakati ibada ya mazishi ya Mariam ikiendelea baada ya kuonekana akirandaranda nje ya kanisa hilo.

Hayo yameelezwa na mchungaji kiongozi wa AICT  Chang’ombe, Elisha Isebuka kabla ya kuanza kuhubiri.

“Wakati  ibada inaendelea mliona baadhi ya viongozi wakitoka. Kijana anayedaiwa kufanya mambo haya alikuwa akizungukia maeneo haya na sasa amekamatwa. Tuviache vyombo vya dola vifanye kazi," amesema.

Mwili wa Mariam ulikutwa kwenye nyumba ya wageni ya East London, Buza anakodaiwa alikuwa na mchumba wake usiku wa kuamkia Septemba 5, 2018.

Soma Zaidi:

·Sakata la mwanakwaya kufia gesti, ndugu watumiwa meseji za vitisho

Chanzo: mwananchi.co.tz