Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemdhihaki Mtume Muhammad kwa Katuni Afariki

Viks Aliyemdhihaki Mtume Muhammad kwa Katuni Afariki

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

MCHORAJI maarufu wa vibonzo raia wa Sweden ambaye alichora mchoro wa kichwa cha Nabii Muhammad kwenye kiwiliwili cha mbwa amefariki dunia katika ajali ya barabarani.

Lars Vilks alikuwa akisafiri katika gari la polisi ambalo liligongana na lori karibu na Mji wa Markaryd, Kusini mwa Sweden huku maofisa wawili wa polisi walifariki na dereva wa lori alijeruhiwa.

Vilks, mwenye umri wa miaka 75, amekuwa akiishi chini ya ulinzi wa polisi waliomlinda baada ya kupata vitisho vya kuuawa kutokana na kibonzo hicho.

Kibonzo hicho, kilichochapishwa mwaka 2007, kiliwakera Waislamu wengi ambao waliuona uchoraji wa picha ya Nabii kama kukufuru.

Hii ilikuja mwaka mmoja baada ya gazeti la Denmark kuchapisha vibonzo vya Mtume Muhammad.

Polisi bado hawajafichua utambulisho wa wale waliouawa katika tukio hilo la Jumapili, lakini mwenzi wa Vilks amethibitisha kifo chake katika gazeti la Dagens Nyheter.

Taarifa ya polisi ilisema bado haijawa wazi jinsi mgongano wa magari hayo ulivyotokea, lakini awali hapakuwa na kitu chochote kilichoonyesha kuwa kuna mtu yeyote aliyehusika.

Kibonzo hicho kilisababisha hasira kubwa kutoka kwa umma na kusababisha aliyekuwa Waziri mkuu wakati huo, Fredrik Reinfeldt kukutana na mabalozi kutoka nchi 22 za Kiislamu kujaribu kutuliza hali.

Muda mfupi baadaye, kikundi cha al-Qaeda nchini Iraq kilitangaza kutoa $100,000 (£73,692) kama zawadi kwa yeyote atakayemuua.

Mnamo mwaka 2015, Vilks alishiriki mjadala kuhusu uhuru wa kujieleza ambao ulilengwa na shambulio la bunduki katika mji wa Copenhagen. Alisema huenda alikuwa mlengwa wa shambulio hilo, ambalo lilimuua muelekezaji mmoja wa filmu.

Chanzo: globalpublishers.co.tz