Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichosema Mbowe msibani kwa baba mzazi wa Mtume Mwingira

96706 Mbowe+pic Alichosema Mbowe msibani kwa baba mzazi wa Mtume Mwingira

Mon, 24 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibaha. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania Chadema, Freeman Mbowe amewaomba watumishi wa Mungu kuliombea Taifa ili haki iweze kutawala katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.

Mbowe ameyasema hayo leo Jumamosi Februari 22, 2020 wakati wa ibada ya baba mazishi ya Elias Mwingira ambaye ni Baba mzazi wa Mtume na Nabii wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira yanayofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Amesema baraka aliyotupa Mungu ya amani, upendo na mshikamano haupaswi kudharauliwa wala kukufuriwa.

"Ombi maalum kwa Mtume Mwingira, ukaungane na watumishi wengine kuliombea Taifa na viongozi kwa kuwa ndiyo wenye uamuzi wote," amesema Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni nchini humo

"Huu ni mwaka wa uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani, tunaomba Mtume ukaongoze viongozi wengine wa dini kuombea uchaguzi huu," amesema

Amesema kuna haja ya kuombea viongozi wetu wa kisiasa ili waache kiburi.

Pia Soma

Advertisement
"Kuichafua nchi ni rahisi kwa siku moja kama tutaendekeza kuwa na kiburi, haki huinua Taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote,” ameongeza

Naye Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amesema mtu hapaswi kumhukumu mtu mwingine kulingana na jambo alilofanya.

Dk Tulia amesema maandiko matakatifu yanaeleza hupaswi kumuhukumu mtu kwa jambo alilofanya huenda likawa na faida kwa jamii.

Baadhi ya viongozi waliofika katika maziko hayo ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa aliyemwakilisha Rais wa Tanzania, John Magufuli, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Wengine ni; Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii katika awamu ya nne ya Serikali ya Tanzania.

 

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi.

Chanzo: mwananchi.co.tz