Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afya yangu ni nzuri, sitojiuzulu - Papa Francis

Papa Francis Ataka Kuzikwa Nje Ya Vatican Afya yangu ni nzuri, sitojiuzulu - Papa Francis

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis hana nia ya kujiuzulu kwani anahisi afya yake ni nzuri na anaweza kuendelea na majukumu yake.

Mtandao wa @DW_Kiswahili umeripoti kuwa Baba Mtakatifu ameyasema haya katika kitabu kipya ambacho dondoo zake zimechapishwa katika gazeti la Nchini Italia la Corriere della Sera.

Katika kitabu hicho ambacho kinatarajiwa kutolewa rasmi mnamo March 19, Papa anasema wazo la kujiuzulu ni ndoto kwakuwa hana sababu yoyote ya kumpelekea kufanya hivyo.

Francis mwenye umri wa miaka 87 katika miaka ya hivi karibuni ameripotiwa kuugua mara kadhaa, ambapo amekuwa akitumia kiti cha magurudumu au mkongojo kutembea, amekuwa akiugua mafua mara kwa mara jambo lililompelekea kupunguza maongezi yake mbele ya umma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live