Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afya ya Papa Francis yaimarika baada ya kulazwa hospitalini usiku

Afya Ya Papa Francis Yaimarika Baada Ya Kulazwa Hospitalini Usiku Afya ya Papa Francis yaimarika baada ya kulazwa hospitalini usiku

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Afya ya Papa Francis inazidi kuimarika baada ya kufikishwa hospitalini akiwa na hali iliyoonyesha matatizo ya kupumua, Vatican imethibitisha.

Alilazwa katika Hospitali ya Gemelli siku ya Jumatano, kwa kile kilichosemekana kuwa ni uchunguzi uliopangwa kufanyika.

Katika taarifa yake siku ya Alhamisi, msemaji wa Vatican Matteo Bruni alisema matibabu ya papa huyo mwenye umri wa miaka 86 yanaendelea.

"Mtakatifu Papa Francis alipumzika vizuri wakati wa usiku," alisema.

"Leo asubuhi baada ya kifungua kinywa, alisoma baadhi ya magazeti na kuanza kazi tena."

Aliongeza kuwa kisha alikwenda katika kanisa la hospitali hiyo, ambako alisali na kupokea Ekaristi.

Bw Bruni hakusema ni lini Papa anaweza kuondoka katika hospitali ya Gemelli ya Roma. Vatican ilisema Jumatano alitarajiwa kukaa "siku chache" huko.

Wafanyakazi wake wa karibu, wakiwemo wa usalama, walilala naye usiku kucha, mtu mwenye ufahamu wa moja kwa moja aliambia BBC.

Huu ni wakati wenye shughuli nyingi zaidi za mwaka kwa Papa Francis, huku matukio na ibada nyingi zikipangwa kabla ya wikendi ya Pasaka.

Misa ya Jumapili ya matawi inafanyika wikendi hii, huku Wiki Takatifu na sherehe za Pasaka zikifuata wiki ijayo.

Chanzo: Bbc