Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

56 wanusurika kifo boti ikishika moto majini

76060 Boti+pic

Tue, 17 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Muleba.  Watu 56 wamenusurika kifo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria katika ziwa Victoria mkoani Kagera kuwaka moto.

Boti hiyo ilikuwa ikitoka Wilaya ya Bukoba kwenda Rushonga wilayani Muleba.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 17, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema boti hiyo iliyokuwa na abiria 56 pamoja na mizigo, ilianza safari jana mchana Jumatatu Septemba 16, 2019 lakini baada ya muda mfupi ilishika moto, kugeuzwa kurejea bandarini.

Amesema abiria wote waliokuwa katika boti hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 84 waliokolewa na watu waliokuwa ufukweni, baadhi waliweza kuogelea wenyewe.

“Majeruhi watatu walikimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph Kagondo, kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri,” amesema kamanda huyo.

Michael Dominick, mkazi wa Isamilo aliyeshuhudia tukio hilo amesema boti hiyo ilianza kuwaka moto muda mfupi baada ya kuondoka bandarini, “Ulitokea mlipuko eneo la nyuma la boti katika injini na kusababisha moto mkubwa.”

Pia Soma

Advertisement

“Abiria walipiga kelele kuomba msaada na wengine waliruka katika maji na kuogelea.”

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco  Gaguti amewapa pole wananchi hao, kuwataka kuhakikisha wanazingatia usalama wao wakati wa kusafiri sambamba na wakaguzi wa vyombo vya majini kufanya ukaguzi.

“Wananchi mtusaidie Serikali kwa kuhakikisha mnavikagua vyombo hivi kabla ya safari mkivitilia mashaka toeni taarifa kwa mamlaka husika ili tuweze kudhibiti ajali hizi kabla ya kutokea,” amesema mkuu huyo wa Mkoa.

Gaguti na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo umewatembelea majeruhi watatu wa ajali hiyo.

Majeruhi hao ni Elizabeth Msiwa (28), Agnes Wiliam (42) na Mariam Deus (30).

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz