Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'waliowapiga viongozi wa Kijiji wakamatwe'

220d1d267e50d2408fc8bdd161f9ace9 DC akizungumza na wananchi wa Tanganyika

Fri, 20 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Onesmo Buswelu, ameliagiza Jeshi la Polisi wilaya humo, kumkamata mfugaji aitwaye Runyalaja Omari na wenzake wanaodaiwa kuwafanyia fujo, ikiwemo kuwapiga viongozi wa kijiji cha Karema.

Tukio hilo inadaiwa lilitokea wakati wakizuia ng'ombe za mfugaji huyo, kuharibu alizeti katika shamba la mkulima wa kijiji hicho.

Buswelu ametoa agizo hilo alipofika katika kijiji hicho kwa lengo la kuangalia maendeleo ya ukarabati wa ujenzi wa kituo cha afya Karema na kukuta baadhi ya wananchi wakimsubili katika kituo hicho, ikiwemo waathirika wa tukio hilo, ambao ni Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijiji.

Amesema hakuna njia nyingine zaidi ya kuwakamata watu hao na kuchukua hatua za kisheria.

"Awe aliyekuwa anachunga, awe mmiliki wa mifugo, mama au baba wote lazima muwakamate, uwezo wa kuwakamata si mnao?

“Tuna OCS, tuna jeshi la akiba, tuna kamati ya usalama ya kijiji shirikianeni kamateni wote,"amesema Buswelu.

Kwa mujibu wa waathirika wa tukio hilo, wanasema walikwenda eneo hilo kushughulikia ng'ombe zinazokula mazao ya wananchi, hivyo walikuta ng'ombe zaidi ya 500 zikila alizeti katika shamba la mwananchi.

Lakini wakati wakifukuza ng’ombo hao, walianza kushambuliwa ikiwemo fimbo kichwani na kwamba tukio hilo si la kwanza kutokea katika kijiji hicho likimuhusisha mfugaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live