Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

mbaroni kuanzisha kiwanda feki cha sukari Songwe

A2289C0B 3375 4897 A81F F7532DDD5999.jpeg mbaroni kuanzisha kiwanda feki cha sukari Songwe

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Wafanyabiashara watano wakazi wa Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe wanashikiliwa Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kukutwa na sukari ilioghushiwa na kufanana na nembo ya Kiwanda cha Sukari cha Kampuni ya Kilombero.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa ACP Alex Mukama amewataja waliokamatwa ni pamoja na Oscar Chisunga (35), John Chisunga (36), Moses Mussa (36) ,Fredy Thobias (28) na Eddy Mwashambwa (44) ambapo wamekutwa na kilo 440 za sukari zinazodaiwa kuingizwa nchini kimagendo na kuwekwa kwenye mifuko ya sukari kutoka viwanda vya ndani ya nchi.

Watuhumiwa hao pia wanadaiwa kukutwa na mashine tatu tofauti zinazotumika kufungasha bidhaa za sukari, mikasi mitatu, mifuko mitupu 110 ya sukari ya Kg50 ya kampuni ya SALIM SUGAR CO.LTD ya nchi kutoka nchi jirani.

Pia wamekutwa na mifuko mitupu 44 ya sukari kilo 20 ya Kampuni ya TSEKETSEKE ya ILLOVO SUGAR ya nchi jirani, mifuko mitupu mitatu ya sukari ya kilo 20 ya Kampuni ya KILOMBERO SUGAR COMPANY na vifungashio vya Sukari 1,164 vya ujazo wa kilo 1 kila kimoja na rola moja lenye nembo ya sukari ya KILOMBERO SUGAR COMPANY .

Kamanda Mukama amesema kuwa Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali imefanya operesheni maalumu ya Polisi iliyofanyika kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Bodi ya Sukari Tanzania na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero ndiyo imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa.

Tayari uchunguzi unaendelea kubaini wahusika wengine kutoka kiwanda cha Sukari Kilombero ambao wanashirikiana na watuhumiwa kutoa nyaraka za Kampuni kama vifungashio na mifuko yakubebea Sukari. Ametoa wito kwa wananchi wote kutokujihusisha na shughuri za kuhujumu viwanda vyetu vya ndani kwani huo ni uhujumu wa Uchumi wa viwanda na taifa kwa ujumla.

Chanzo: Mwananchi