Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

machinga wavamia kikao cha Baraza la Madiwani

Wavamiapic Wamachinga wavamia kikao cha Baraza la Madiwani

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) wamevamia kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Iringa wakitaka hoja dhidi ya hatma ya eneo lao la kufanyia biashara ijadiliwe.

Hata hivyo, Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada amesema kwa mujibu wa sheria za baraza hilo, hoja hiyo binafsi imechelewa kuwasilishwa kwani ilipaswa kufikisha siku nne kabla.

"Hatuwezi kujadili hoja iliyokuja nje ya utaratibu, kanuni haziruhusu," amesema Ngwada.

Ngwada amefunga vikao vya baraza hilo na kuahidi kuwa hoja ya machinga hao itaongelewa baadaye. Diwani wa Kata ya Mlandege, Jackson Chaula ndiye aliyetaka kuwasilisha hoja hiyo.

Katibu Mtendaji wa Umoja wa Wamachinga Iringa, Joseph Kilyenyi amesema waliomba madiwani wajadili hoja yao wakitaka wapewe eneo la Mlandege ambalo kwa sasa lina makaburi ya zamani.

"Tuliomba madiwani wazungumzie lile eneo la Mlandege lenye makaburi ya zamani. Linaweza kubadilisha matumizi," amesema Ngwada.

Chanzo: mwananchidigital