Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuberi Kidumo Meya mpya manispaa ya Moshi

Meya Mpya Moshi Zuberi Kidumo Meya mpya manispaa ya Moshi

Thu, 30 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diwani wa Kata ya Njoro, Zuberi Kidumo (CCM) amechaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Moshi, kurithi mikoba ya aliyekuwa meya wa Manispaa hiyo Juma Raibu.

Akitangaza matokeo katika uchaguzi huo ambao umefanyika leo Ijumaa Juni 30, 2022, mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Rashid Gembe amemtangaza Kidumo kuwa mshindi kwa kupata kura 27 kati ya kura 28 zilizopigwa ambayo ni sawa na asilimia 96.4 huku Diwani wa Kata ya Kiboriloni, Frank Kagoma (Chadema) akipata kura moja.

Nafasi hiyo ilikuwa wazi kuanzia Aprili 11, 2022 baada ya aliyekuwa meya wa Manispaa hiyo, Juma Raibu kung'olewa katika wadhifa huo na madiwani wakimtuhumu kwa tuhuma mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live