Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zoezi la ufunguaji mitaa Kateshi, Hanang lafikia asilimia 85

N 3 1 Kateshi, Hanang Zoezi la ufunguaji mitaa Kateshi, Hanang lafikia asilimia 85

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema zoezi la ufunguaji wa mitaa katika mji wa Kateshi limefika asilimia 85 na mkazo mkubwa umewekwa katika kutoa udongo kwenye vipenyo vya vya mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama katika mahojiano maalumu aliyoyafanya na shirika la utangazaji la Taifa TBC jaana tarehe 13/12/2023 Hanang Manyara.

Waziri alisema katika zoezi hilo malori makubwa zaidi ya 30 yalisaidia kutoa tope lenye mawe miti pamoja na udongo, katika barabara kuu ya Katesh Singida. “Malori yenye uwezo wa kubeba magunia 130 yamefanya safari zaidi ya 400 ya kutoa Tope kutoka kwenye viunga vyote vya Mji wa Katesh,” alibainisha.

Waziri amefafanua kwamba, vifaa tulivyonavyo haviwezi kuingia kwenye vipenyo vya mtaa kwa mtaa au nyumba kwa nyumba na hivyo tunalazimika kutumia nguvu kazi, na tunafanikiwa.

Halikadhalika tunafikiria kushirikisha wananchi kujitokeza kusaidia zoezi la uondoaji wa tope hasa kwenye hifadhi ya barabara ili tuweke hali katika usalama zaidi.

“Tunafanya tathimini na kuendelea kuchukua tahadhari mvua nyingine ikinyesha, ikiwa ni pamoja na kurudisha mto uliopokea mawe na matope ambao njia yake ilifunga na kutengeneza mapito mengine,” alifafanua.

Kwa upande wake Mkazi wa Katesh,  Halima Rashidi amesema Mawe na tope yaliyoletwa na Mlima Hanang yaliathiri kwa kiasi kikubwa miundo mbinu na makazi ya watu.

“Msaada wa serikali umekuja kwa wakati na haraka, watu wana moyo wa kufanya kazi kwa sababu jitihada zao zimeokoa maisha ya watu na mali,” alibainisha

Chanzo: www.tanzaniaweb.live