Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ziwa Victoria lina boti ‘bubu’ zaidi ya 250

3f8408d6fdf186fd6428aaea89666a9a.jpeg Ziwa Victoria lina boti ‘bubu’ zaidi ya 250

Fri, 22 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imebaini kuwapo zaidi ya boti bubu 250 katika Ziwa Victoria zinazotoa huduma mbalimbali mkoani Geita, ikiwamo kusafirisha abiria na uvuvi bila ya kusajiliwa.

Akizungumza kwenye kampeni maalumu ya kutoa elimu ya kanuni za usalama wa vyombo vya usafirishaji majini katika mialo ya Nkome, Mchangani na Makatani, wilayani Geita juzi, Ofisa Mfawidhi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) mkoani Geita, Rashid Katonga alisema boti hizo zinakiuka kanuni, taratibu na sheria zinazosimamia usafiri wa majini nchini.

Alisema mkoa wa Geita unakadiriwa kuwa na zaidi ya boti 1,000 zinazotoa huduma ya usafirishaji katika Ziwa Victoria.

“Boti 750 zikiwamo za uvuvi pamoja na zinazosafirisha abiria na mizigo ndizo zimesajiliwa, hivyo kufanya kazi zake kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria.”

“Kutosajiliwa kwa zaidi ya boti 250 kumeilazimu TASAC kutoa elimu kwa wamiliki wake kuhusu umuhimu wa kuthibitishwa kwa ubora wa vyombo vyao,” alisema.

Katonga aliwataka wamiliki wa boti hizo kuzisajili haraka kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Akitoa elimu kwa wananchi jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Emmanuel Ndomba alisema kuna mpango wa ujenzi wa vituo 10 vya kuratibu shughuli za ufuatiliaji na uokoaji katika Ziwa Victoria.

Chanzo: habarileo.co.tz