Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimamoto Mbeya wadai ujenzi holela unawakwamisha

Zimamoto.jpeg Zimamoto Mbeya wadai ujenzi holela unawakwamisha

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya, limesema litaendelea kutoa elimu ya mara kwa mara juu ya jamii kuacha wazi maeneo ya wazi ili janga la moto au jingine linapotokea iwe rahisi kufikika.

Kauli hiyo imetolewa leo, Alhamisi Januari 18, 2024, Kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa, Malumbo Ngata alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya utendaji kazi wao ambapo amesema kwa kipindi cha miezi sita iliyopita, zaidi ya matukio 53 yaliripotiwa yakiwemo ya moto 46 na vifo viwili vya watoto waliotumbukia kwenye visima vya maji.

“Unajua kuna baadhi ya maeneo wamejenga kiholela makazi, likitokea tukio la moto namna ya kufanya uokoaji ni tabu, inatulazimu kutumia akili nyingi ya ziada ya namna ya kupitisha vifaa na na magari,” amesema.

Ngata amesema bado kuna uelewa mdogo wa jamii katika kuona umuhimu wa kuacha maeneo ya wazi, hivyo inawalazimu kutoa elimu ya mara kwa mara

“Kuna kazi kubwa ikiwepo elimu kwa jamii hususani kwenye ngazi za familia kwani kuna baadhi ya matukio chanzo chake ni uzembe wa watoto kutumia mishumaa, kwa mfano kwenye maeneo ya shule,” amesema.

Kamanda huyo amesema kutokana na changamoto hiyo, wamekuwa kushirikiana na ofisi za mipango miji wakishauriana ili kuhakikisha miundombinu ya barabara inakuwa rahisi ili kuyafikia maeneo.

Amesema ili kukabiliana na matukio kwenye maeneo ya shule wamefanya ukaguzi mara kwa mara wa mabweni kuhakikisha yanakuwa na vifaa vya kuzimia moto sambamba na kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi ili kuzuia ajali za moto.

Kwa upande wake, mkazi wa Mabatini, Lucy Aloyce amekiri ujenzi holela kuwa ni changamoto kubwa kwenye majanga ya moto na shughuli za kijamii ikiwepo harusi na misiba.

“Kuna baadhi ya mitaa haina mpangilio mzuri wa makazi, hivyo Serikali inapaswa kuchukua hatua ya kudhibiti ujenzi holela wa makazi,” amesema.

Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Mapinduzi, Reuben Fredy ameomba elimu itolewe ili waepukane na majanga ya moto na matumizi ya vitu hatarishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live