Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimamoto Airport waingia kuzima moto Mwanza Hotel

Zimamoto Pic Data Zimamoto Airport waingia kuzima moto Mwanza Hotel

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati moto umeteketeza Casino ya Dallas iliyoko ndani ya Mwanza Hotel jijini Mwanza usiku wa jana.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima alilazimika kuagiza magari ya kuzima moto kwenye viwanda na uwanja wa Ndege mkoani Mwanza kuletwa kukabiliana na moto huo.

Hata hivyo, haikuchukua dakika zaidi ya 10 kabla gari la kuzima moto kutoka uwanja wa ndege mkoani Mwanza likawasili na kuongeza nguvu kukabiliana na moto huo.

Pamoja na magari hayo, bado moto huo uliendelea kuwaka na kuteketeza eneo la klabu hiyo huku juhudi za kupambana kuuzima zikiendelea.

Kwa upande wa mashuhuda wa tukio hilo, Jeshi la Polisi liliendelea kuwatuliza na kuwahimiza kukaa mbali na moto huo ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live