Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya watu 40 wafariki ajali ya moto

353525f027c48e761b5f594f4c6d6b71 Zaidi ya watu 40 wafariki ajali ya moto

Thu, 14 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Watu wasiopungua 46 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya moto kuwaka kwenye jengo moja lililopo Kusini kwa Taiwan leo Oktoba 14, 2021.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la CNA la China, moto huo ulianza asubuhi katika jengo la biashara la ghorofa 13 Wilaya ya Yancheng, ambapo zaidi ya maafisa wa ukoaji 337 wanaendelea na shughuli za uokoaji.

Msemaji wa kikosi cha zima moto mji wa Kaohsiung aliambia CNN kuwa zaidi ya watu 41 wamejeruhiwa na kuonya kuwa huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka zaidi kutokana na baadhi yao kunasa kwenye jengo.

Taarifa za awali, haijafahamika chanzo cha moto huo, ambapo kwa mujibu wa CNA polisi wameanza uchunguzi kwa kupitia baadhi ya mikanda ya video

Chanzo: www.habarileo.co.tz