Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya robo hawajaripoti shuleni Kondoa

Wanafunziiiiiiiiiii Utoro.jpeg Zaidi ya robo hawajaripoti shuleni Kondoa

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi 593 kati ya 1,782 wa kidato cha kwanza waliopangiwa katika halmashauri ya mji wa Kondoa mkoani Dodoma hawajaripoti shuleni hadi kufikia jana.

Kwa mujibu wa halmashauri ya mji huo, walioripoti 1,189 na uongozi wa Mkoa wa Dodoma ulijiwekea lengo kuwa mwisho wa kuripoti kwa wanafunzi ni Januari 16, 2024.

Ofisa uhusiano wa halmashauri ya mji wa Kondoa, Sekela Mwaisubila amesema katika shule ya sekondari ya Serya waliopangiwa walikuwa ni 184 lakini walioripoti walikuwa ni 92 huku Mto Bubu waliopangiwa ni 175 wakati walioripoti ni 94.

Akizungumzia hatua zitakazochukuliwa kuhakikisha wanafunzi wanaripoti shuleni, Ofisa Elimu wa mkoa wa Dodoma, Vicent Kayombo amesema watendaji wamepatiwa majina ya wanafunzi na mahali wanapoishi kwa ajili ya kuwafuatilia.

“Wazazi waliowapeleka watoto wao katika shule binafsi wawe na barua za kuonyesha kuwa wamepelekwa katika shule hizo ili watendaji watakapopita wathibitishe hilo,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live