Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya miche 5,000 mikarafuu yatolewa bure

MIKARAFUU Zaidi ya miche 5,000 mikarafuu yatolewa bure

Tue, 28 Apr 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ZAIDI ya mikarafuu 5,000 imekabidhiwa kwa Masheha wa Wilaya ya Kaskazini B kwa ajili ya kuwapa wananchi waliopo katika shehia za wilaya hiyo kuendeleza kilimo hicho nchini.

Akikabidhi mikarafuu na kuzindua upandaji wa mikarafuu hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Rajab Ali Rajab, alisema mikarafuu hiyo inatolewa bure kwa wananchi ili kukiendeleza na kukikuza kilimo kwa kuzalisha zao hilo kwa wingi.

Alisema kilimo hicho kina faida na wananchi wanaweza kupata kipato kitakacho wakomboa na umaskini kupitia zao hilo endapo wananchi hao watatilia mkazo kama ilivyo kwa kilimo kingine.

Alisema katika kisiwa cha Unguja, wilaya ya Kaskazini B ndiyo inayoongoza kwa uzalishaji wa karafuu na sasa mikakati yao ni kuhakikisha wanaifuatilia kwa kila mwananchi aliepatiwa ili mwakani kujua mingapi iliyoweza kukuwa vizuri.

Aliwataka Masheha kushirikiana na wataalamu wa kilimo ili kila mwananchi atakaepatiwa miche hiyo aweze kufuatiliwa na kujua maendeleo ya ukuaji wake na namna ya kuitunza.

Naye Msaidizi Mkurugenzi wa sekta ya kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B, Suleiman Khamis, alisema, matarajio yao kwa mwaka ujao ni kuzalisha zaidi ya mikarafuu 40,000 katika kitalu ili kukuza kilimo hicho ndani ya wilaya hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live