Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya kaya elfu 30 zapata maji Mbezi

Kero Majipic Zaidi ya kaya elfu 30 zapata maji Mbezi

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya kaya elfu 30 za Mbezi Makabe na viunga vyake wilayani Ubungo mkoani Dar es Salaam zimeanza kupata huduma ya maji safi na salama baada ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuboresha miundomhimu ya kuongeza msukumo wa maji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Kiula Kingu amesema,, hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Maji Jumaa Aweso la kutaka kufikishwa kwa huduma ya maji katika maeneo ambayo hayajapata maji ili kutimiza azma ya Serikali ya kumtua ndoo Mama kichwani.

Katika hatua nyingine Kingu amewataka Wananchi wasio na uwezo wa kulipia maji ili kuunganishiwa kufika katika ofisi za DAWASA zilizopo karibu, ili waweze kuunganishiwa huduma hiyo kwa mkopo.

Wakizungumza na TBC wakazi wa maeneo hayo wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikishia huduma ya maji, kwani walikuwa wananunua maji ya shilingi elfu 60 kwa wiki na hivyo kuongeza gharama za maisha.

Maboresho ya miundombinu hiyo katika miradi ya maji yameigharimu Serikali zaidi ya shilingi Bilioni moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live