Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya ekari 3000 za bangi zateketezwa Tarime

Bangi Shambaaa (600 X 349) Zaidi ya ekari 3000 za bangi zateketezwa Tarime

Thu, 10 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Polisi, Jeshi la Akiba na Wananchi, imefanya oparesheni kubwa ya wiki tatu katika Wilaya ya Tarime na Serengeti Mkoani Mara kukabiliana na uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya aina ya bangi na kufanikiwa kuteketeza jumla ya ekari 3,007 za mashamba ya bangi huku kilogramu 7,832.5 za bangi kavu na kilogramu 452 za mbegu za bangi zikikamatwa.

Oparesheni hiyo imefanyika katika Vijiji vya Matongo, Nyarwana, na Weigita vilivyopo Bonde la Masinki, pia vijiji vya Nkerege, Kembwe, Nyakunguru na Iseresere pamoja na eneo la Bonde la Mto Mara ambapo Watuhumiwa 17 wamekamatwa wakati wa oparesheni hiyo na tayari wamefikishwa Mahakamani.

Akiongea baada ya oparesheni hiyo jana October 08,2024, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo, amesema oparesheni hii ni sehemu ya jitihada za Serikali kulinda jamii dhidi ya madhara ya dawa za kulevya.

“Mamlaka imebaini kuwa kilimo cha bangi Mkoani Mara kinafadhiliwa na Raia wa Nchi jirani ambao huwapa mitaji Wakulima wa Tarime kisha bangi ikishakomaa huvunwa na kusafirishwa kwenda kuuzwa, tunatoa miezi mitatu kwa Wananchi wa Mara kuhakikisha wanaacha kabisa kujihusisha na kilimo cha bangi, baada ya muda huo, tutafanya oparesheni kubwa kwa namnna nyingine na kuhakikisha maeneo haya yanabadilishiwa matumizi na hayatumiki tena kwa kilimo cha bangi, pia wote wanaotetea uhalifu huu watachukuliwa hatua ili kuhakikisha Wananchi wote wanatii sheria za Nchi”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live