Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya asilimia 60 ya wanaume Katavi hawajatahiriwa

97720 Wanaume+pic Zaidi ya asilimia 60 ya wanaume Katavi hawajatahiriwa

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katavi. Zaidi ya asilimia 60 ya wanaume mkoani Katavi hawajatahiriwa na wengine wanadaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja hali inayosababisha kuongezeka kwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi. Mratibu wa ukimwi mkoa hapa, Alex Mrema akizungumza leo Jumatatu, Machi 2, 2020kwenye  kikao na wadau wa afya cha  kujadili namna ya kutokomeza maambukizi mapya ya VVU, amesema hali hiyo imesababisha mkoa kushika nafasi ya pili kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ukiwa na asilimia 5.9, Mbeya ikishika nafasi ya kwanza ikiwa na asilimia 9.4. "Chanzo kikubwa cha tatizo hili ni wanaume wengi kutotahiriwa, wengine wameoa zaidi ya mwanamke mmoja, wapo watatu tumewabaini wanafanya mapenzi ya jinsia moja kati yao mmoja ameathirika tumempa ushauri nasaha na kumwanzishia matibabu na wawili tumewapa kinga. Mbali na hao ametaja makundi mengine yanayoeneza ugonjwa huo ni madereva wa magari ya masafa marefu, wanawake wanaofanya biashara ya ngono, wafanyakazi wa baa na vijana walio katika umri wa kubalehe wanaojihusha na mapenzi. Mrema amesema katika mkoa wa Katavi watu waliogundulika kuwa na maambukizi ni 23,000, lakini walioingizwa kwenye mfumo wa matumizi ya dawa za kufubaza ni 20,000 tu na 3,000 hawajulikani walipo," amesema Mrema. "Ili kutokomeza janga hili tumeanzisha kampeni ya kupima VVU nyakati za usiku, tutayafikia maeneo yote yaliyo na mkusanyiko wa watu ili tuwapate hawa 3,000 ambao hawajulikani walipo." Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Mkoa wa Katavi, Justina Tizeba amesema kampeni ya kupima usiku ni utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kufikia tisini tatu ifikapo 2020. "Tumekutana leo hapa kutambulisha kampeni yetu ya upimaji nyakati za usiku moonlight testing ili kutokomeza janga hili hususani kwa makundi hatarishi tuliyoyabaini," amesema Tizeba. Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, ofisa elimu shule za sekondari Manispaa ya Mpanda, Enelia Lutunguru amesema kundi la wanafunzi limesahaulika wakati ndiyo wahanga wakubwa. "Mafunzo haya wangepatiwa na wanafunzi kwa sababu wengi wanafanya mapenzi bila kutumia kinga, hawazifahamu hata kondomu wangekuwa wanatumia wasingekuwa wanapata ujauzito,"amesema Lutunguru.

Chanzo: mwananchi.co.tz