Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya Bilioni 4 zaokolewa Njombe

Njocoba Ed Zaidi ya Bilioni 4 zaokolewa Njombe

Thu, 11 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI mkoani Njombe imeokoa zaidi ya Bilioni 4 kati ya Bilioni 7.9 zilizokuwa hatarini kutafunwa na baadhi ya watu waliokuwa wamekopa fedha kutoka katika Vyama vya Ushirika na Benki ya Wananchi Njombe (NJOCOBA) na kushindwa kuzirejesha mpaka serikali ilipoingilia kati.

Kwa mujibu wa taarifa za serikali zimesema kuwa kiasi cha Bilioni 1.48 za NJOCOBA na zaidi ya Bilioni 6.5 zilikopwa kutoka katika vyama vya ushirika na kutokomea nazo jambo ambalo likasababisha vyama vingi vya ushirika kufa na vingine kujiendesha kwa kusuasua.

Hata hivyo kutokana na kitendo cha benki ya wananchi kufilisika ni kwa sababu ya fedha nyingi kukaa mikononi kwa baadhi ya watu waliokopa kulimsukuma Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Olesendeka kuanza kufatilia madeni hayo na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Bilioni 4 ambazo zipo kwenye utaratibu wa kurejesha kwa wananchi kwa utaratibu maalumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live