Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wotesawa yaokoa watoto 57 kutoka kazi za nyumbani

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Watoto 67 wenye umri chini ya miaka 14 waliokuwa wakifanya kazi za nyumbani waliokolewa na kuunganishwa na familia zao huku wengine 82 wakisaidiwa kupata mikataba bora ya ajira kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Mratibu wa Shirika la Wotesawa linalotetea wafanyakazi wa nyumbani, Elisha David amesema zaidi ya wafanyakazi wa nyumbani 1,000 walipewa mafunzo ya kutambua haki na wajibu wao kazini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha utoaji wa huduma na msaada wa kisheria kwa wafanyakazi wa nyumbani unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Mkurugenzi Mtendaji wa WoteSawa, Angela Benedicto amesema licha ya ujira mdogo, baadhi ya wafanyakazi wa ndani pia hufanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji.

“Kwa kushirikiana na wadau wengine tutaelimisha umma kukomesha ukatili na unyanyasaji kwa wafanyakazi wa nyumbani,” amesema Angela.

Mwanasheria wa Shirika hilo, Joseph Mukoji amesema mradi huo wa miezi sita unaotekelezwa katika wilaya za Ilemela na Nyamagana kwa gharama ya zaidi ya Sh49 milioni utawafikia watu zaidi ya 440 kupitia elimu ya kutambua haki, usuluhishi na msaada wa kisheria.



Chanzo: mwananchi.co.tz