Thu, 5 Jan 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, limewaonya wananchi na wafanyakazi wanaojihusisha na vitendo vya wizi wa vifaa vya ujenzi katika mradi wa daraja la JPM Magufuli linalojengwa eneo la Kigongo - Busisi mkoani Mwanza.
Daraja la JPM Magufuli lenye urefu wa kilomita 3.3 linajengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 700.
Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa wakati wa doria ziwa Victoria iliyolenga kuendelea kulinda amani Ziwani.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live