Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yasitisha mpango halmashauri kujimilikisha eneo la uwekezaji

Geophrey Mizengo Pinda Wizara yasitisha mpango halmashauri kujimilikisha eneo la uwekezaji

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda amesitisha mara moja mpango wa Halmashauri ya Wilaya ya Same kuchukuwa eneo la wananchi wa kijiji cha makanya lenye ukubwa wa Ekari 4,000 lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda bila kushirikisha wananchi hao kwa madai kuwa ni wawekezaji.

Pinda ametoa kauli hiyo Wilayani Same mkoani Kilimanjaro leo tarehe 16 Agosti 2023 wakati alipofanya kikao na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same na kubaini mpango huo wa Watumishi wa umma kujigeuza wawekezaji katika eneo hilo kwa kujimilikisha kwa gharama zisizokuwa na tija.

Kitu cha ajabu ni kwamba watumishi wa umma mmegawana ekari 4,000 kwa kupangisha kila mmoja ekari 25 kwa malipo ya shilingi milioni moja tu kwa kipindi cha miaka 20 hadi 25, yaani kiasi hiki cha fedha kwa watumishi mnaojiita wawekezaji hakina tija yoyote kwa Taifa Amesema Naibu Waziri Pinda.

Pinda amesitisha mpango huo wa watumishi wa Serikali kujimilikisha eneo lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na badala yake kulifanya kuwa la kilimo bila makubaliano ya wananchi huku watumishi wa umma kujigeuza wawekezaji jambo ambalo lilipingwa na wananchi wa eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live