Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yaeleza sababu sato kufa Ziwa Muhazi

517953d423eec2875133967c867f2b45.jpeg Wizara yaeleza sababu sato kufa Ziwa Muhazi

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WIZARA ya Kilimo imeeleza kuwa samaki 3,700 aina ya sato waliokufa katika Ziwa Muhazi Januari 17 walikosa hewa ya oksijeni katika eneo hilo.

Ziwa hilo linakadiriwa kuwa takribani samaki 10,000.

Maofisa wa wizara hiyo waliotembelea ziwa hilo kuangalia hali ilivyo walieleza kuwa, mvua kubwa zilizonyesha zilisababisha mmomonyoko wa udongo ambao ulisababisha maji safi kutofika katika eneo hilo na kusababisha kupatikana hewa kidogo ya oksijeni.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo kwenye mtandao wake wa twitter ilieleza kuwa, katika kupata ufumbuzi wa tatizo hilo imepeleka samaki katika upande wenye maji mengi kutoka mita 6.6 mpaka mita 8.2 ambao upepo unaruhusu maji kuingia.

Baadhi ya mashuhuda wameeleza samaki hao walianza kufa Januari 17 majira ya saa 2:00 asubuhi katika bwawa la samaki linalomilikiwa na Haguruka Dukore ambacho ni chama cha vijana 18 kutoka eneo la Mununu, wilaya ya Rwamagana.

Rais wa chama hicho, Aimable Musengamana alisema samaki hao walifugwa kwa miezi sita na walipanga kuwavua Januari 20, mwaka huu.

“Tumepata hasara kubwa kwani awamu ya kwanza tulivuna samaki wenye thamani ya takribani faranga milioni tano.”

“Tuliwekeza fedha zote tulizokuwa nazo kwa kununua chakula na hatukubaki na kitu, hii ni hasara kubwa,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz