Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Maji yanunua magari 25 mradi wa visima virefu

Majiipic Datattt Wizara ya Maji yanunua magari 25 mradi wa visima virefu

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahindi amesema Serikali imenunua magari 25 yatakayotumika kuchimba visima virefu vya maji nchini ambayo tayari imeanza kusambazwa mikoani.

Mhandisi Mahundi amesema leo Alhamisi Septemba 8 ,2022 baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge,  Sahili Nyazabara kuzindua Mradi wa Maji wa  Sangambi ulioghalimu Sh599 milioni  kupitia Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya uviko 19 na kusimamiwa na Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa).

Amesema kuwa lengo la Serikali ni kumtua mama ndoo kichwani, sambamba na kupunguza migogoro ya ndoa, vipigo na manyanyaso kwa kina mama pindi wanapotumia muda mwingi kusaka maji.

''Wizara ya Maji haitalala itafanya kazi usiku na mchana kuona changamoto ya maji inakwisha nchi nzima na kuona kina mama wanapumzika na mateso katika ndoa hivyo nitoe rai tu waendelee kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Mahundi.

Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo ambao ulianza Januari mwaka huu na sasa wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.

''Tunashukuru kwa mradi huu, mimi mwakilishi naomba Serikali kupitia mradi huu huduma ya maji ifike mpaka katika Kijiji cha Shoga na Igumbo ambako kuna changamoto kubwa ya maji safi na salama,'' amesema.

Kwa upande wake Mjumbe wa Mwenge Kitaifa, Zadida Rashid ameshauri kuwepo na mikakati ya mapambano ya VVU na Ukimwi na kwamba watu 200,000 kila mwaka kuambukizwa na hivyo kupoteza nguvu kazi kwa taifa.

Amesema mapambado dhidi ya VVU ni  kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru na kuonya jamii kutowanyanyapaa waathirika   pamoja na wazazi na walezi kuwaepusha vijana na tabia hatarishi zinazoweza kusababisha maambukizi.

Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa), Mhandisi Ismail Nassoro amesema mradi huo una uwezo wa kuzalisha lita 150,000 kwa siku na kuhudumia wakazi 6,776.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Sahili Nyanzabara amesema kuwa mradi huo umekamilka na wananchi wanaanza kupata huduma ya maji licha ya kutoa maelekezo.

''Nimekagua jengo sijaridhishwa na rangi na mifumo ya mitambo ya umeme ambayo inasukuma maji, hivyo nahitaji yafanyike marekebisho ili iweze kudumu kwa muda mfupi,'' amesema.

Aidha amesema kumekuwepo na  changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara  na kusababisha huduma ya maji kuwa hafifu na kuagiza Shirika la Umeme (Tanesco) kusimamia hilo ili huduma ya maji ipatikane usiku na mchana.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz