Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara kuweka taa barabara aliyogoma kuzindua Waziri Mkuu

LIWALE.jpeg Barabara ya Liwale Mjini Mkoani Lindi

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya tukio la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kugoma kuzindua Barabara ya Liwale ambayo kwenye mkataba wa Barabara hio ilipaswa kuwa na taa, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya kwenye Mkutano wa Ndani na Waziri Mkuu amesema tayari mchakato wa kuweka taa hizo umeanza na amemuomba Waziri Mkuu taa zikifungwa akafungue.

"Baada ya tukio la pale Barabarani tumeanza kufanyia kazi, tumeona taa zinazohitajika ni taa 20 na taa hizo zitatoka nje tumeongea na wenzetu wa TANROADS Kufikia mwisho wa mwezi wa 11 tutakuwa tumeweka taa Barabara ya laki inapoanzia na kuhakikisha katikati ya Mji huu taa zote zinawaka ili kwakweli Waziri Mkuu uje kutufungulia hii Barabara"

Itakumbukwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa October 07,2021 akiwa katika ziara yake Mkoani Lindi aligoma kuzindua barabara ya Liwale Mjini ya KM 1.2 kwa sababu haijawekwa taa za barabarani “Mkataba ni kujenga barabara za lami zenye taa, leo mnaniambia nizindue barabara haina taa?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live