Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara kutatua adha ya tembo Kagera

Tembo Chembaaa.jpeg Wizara kutatua adha ya tembo Kagera

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kujenga kituo cha kudumu cha Askari wa Uhifadhi katika Kata ya Kihanga, wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kama sehemu ya mikakati yake ya kupambana na wanyamapori wakali na waharibifu.

Akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mshabaigulu na Kibwera, Kata ya Kihanga Karagwe, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba, amesema ni sehemu ya mikakati ya Wizara katika kutatua migogoro ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa kushirikiana na wananchi.

Aidha Kamishna Wakulyamba ametoa wito kwa wanachi kuendelea kushirikiana na serikali katika kupambana na wananchi wachache wanaoingiza mifugo kwenye Hifadhi za Taifa jambo linalosababisha wanyamapori kukimbia maeneo yao ya asili na kukimbilia kwenye makazi ya watu na kusababisha migogoro.

Awali akimkaribisha Kamishna Wakulyamba kuongea na wananchi, Mbunge wa Jimbo la Karagwe ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameeleza kuwa changamoto ya Tembo kuvamia makazi ya wanavijiji wa Kata ya Kihanga, imekuwa ya mara kwa mara hivyo mpango wa kuwa na askari wa Uhifadhi kwenye maeneo hayo ni wakupongezwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live