Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara kukarabati visima 69 Mradi wa Rasilhema

1cef837372317735d21f5be6145e7a9e Wizara kukarabati visima 69 Mradi wa Rasilhema

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WIZARA ya Maji na Nishati imesema visima 69 vilivyojengwa kupitia Mradi wa Rasilhema vitafanyiwa ukarabati ili kutoa huduma vizuri kwa wananchi.

Waziri wa Maji na Nishati, Suleiman Masoud Makame, alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Pemba, Bakari Hamad Bakari, aliyetaka kujua maendeleo ya visima vya mradi wa Rasilhema yakoje kwa sasa.

Alisema baadhi ya visiwa vinatoa huduma kwa wananchi na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo mbalimbali Unguja na Pemba.

Makame alisema hata hivyo kuwa, baadhi ya visima vilivyochimbwa kupitia mradi huo, vimebainika kutofanya kazi na wizara ipo katika mpango wa kuvifanyia ukarabati ili vizalishe maji.

“Visima 69 vimechimbwa katika mradi wa Rasilhema, lakini baadhi yake havifanyi kazi; wizara inakusudia kuvifanyia ukarabati tena ili kutoa huduma kwa wananchi,” alisema Waziri Makame.

Aidha, alisema tatizo la majisafi na salama kwa baadhi ya maeneo ikiwemo Mjini Magharibi Unguja, linatazamiwa kupatiwa ufumbuzi kutokana na manufaa ya utekelezaji wa mradi wa maji kutoka India.

Kwa mujibu wa waziri, mradi huo ni muhimu kwa wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi na sehemu nyingine kwani utekelezaji wake utakuwa ufumbuzi wa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama.

Chanzo: habarileo.co.tz